Jinsi ya kupika keki

 Hatua kwa hatua jinsi ya kupika keki laini

Mapishi ya keki

Habari za muda huu leo Nina somo fupi Sana la kushea na wewe soma Hadi mwisho leo tunajifunza jisi ya kupika keki

Mahitaji katika mapishi ya keki

👉Unga wa ngano robo kilo

👉Sukari robo kilo (unaweza punguza kidogo)

👉Margarine (blueband) robo

👉Mayai 5 au 6 (kulingana na ukubwa wa yai)

👉Barkingpowder 1 kijiko kidogo Cha chai

👉 Maziwa vijiko 2 vya kula (kama utapenda sio lazma)

👉Vanila 1 kijiko kidogo Cha chai


Matayarisho


👉Weka margarine kwenye chombo kisha ipige(ikoroge had iwe lain) then weka sukari alaf upige had vichanganyike vizuri na viwe lain.

👉Anza kuweka yai moja moja kwenye mchanganyiko wako wa margarine na sukari huku ukiupiga tena hadi mayai yote yaishe. Hakikisha mayai na mchanganyiko wako vimechenganyika vizuri.

👉Chukua unga wako changanya na barkingpowder alaf umimine kwenye mchanganyiko wako wa mayai, margarine na sukari baada ya hapo changanya hadi uakikishe vimechenganyika vizuri wala hakuna mabonge wa unga yaliyobaki.

👉 Ongeza maziwa na vanila kisha ukoroge mchanganyiko wako.


Kuoka:

👉Chukua chombo chako cha kuokea ukipake margarine au mafuta kwa ndani (unaweza ongeza pia kupitisha unga wa ngano kidogo juu ya mafuta uliyopaka ) hii itasaidia kuzuia cake yako ising'ang'anie kwenye chombo chako ulichotumia kuoka

👉Mimina mchanyiko wako kwenye chombo chako kisha fanya kama una kipiga piga chin taratibu ili kuondoa hewa.

👉Oka keki yako kwenye oven au jiko la mkaa( kwa jiko la mkaa toa mkaa kwenye jiko ubakize kidogo then ubandike sufuria ambalo ndan yake kutakuwa na chombo chako chenye mchanganyiko alafu kwa juu ule mkaa ulioutoa uweke kwa juu kama vile unapalia wali. 

👉Baada ya dakika 45-60 funua uangalie kama keki yako ineiva(utajua kama imeiva kwa kuichoma na kijiti katikati alaf kikatoka kikiwa kikavu.

 ðŸ‘‰Ipua subiria ipoe kidogo uitoe kwenye chombo chako alaf usubirie ipoe kabisaa kwaajiri ya kuanza kuipamba kulingana na mahitaji yako

Post a Comment

Previous Post Next Post